MADRID YAJIWEKA KATIKA HATARI YA KUTIMULIWA KOMBE LA MFALME.
KIUNGO wa Real Madrid, Denis Cheryshev amesisitiza kutopokea taarifa yeyote kutoka klabu yake ya zamani au Shirikisho la Soka la Hispania kumfahamisha alikuwa bado katika adhabu katika mchezo wa Kombe la Mfalme dhidi ya Cadiz uliochezwa jana. Cheryshev ambaye alifunga bao la kuongoza katika ushindi mabao 3-1, alikuwa na kadi tatu za njano katika klabu yake ya zamani ya Villarreal katika michuano hiyo msimu uliopita ambazo zinamfanya kupata adhabu ya kutocheza mechi moja msimu huu. Lakini nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye aliichezea Villarreal kwa mkopo msimu uliopita amesisitiza hajapata taarifa yeyote kuhusiana na adhabu hiyo. Klabu ya Cadiz imethibitisha kuwa wanatarajia kutuma malalamiko yao rasmi kuhusiana na tukio hilo ambalo linaweza kupelekea Madrid kuondolewa katika michuano hiyo. Klabu ya Osasuna walienguliwa katika michuano ya Kombe la Hispania Septemba mwaka huu baada ya kumtumia mchezaji Unai Garcia ambaye alikuwa katika adhabu.
No comments:
Post a Comment