MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amepanga kumtuliza Divock Origi baada ya nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji kuanza kuonyesha makali yake kwa kupiga hat-trick katika mchezo dhidi ya Southampton. Origi mwenye umri wa miaka 20 alikuwa hajafunga bao katika mechi 10 alizocheza toka ajiunge tena na Liverpool baadae ya kukaa Lille kwa mkopo msimu uliopita. Nyota huyo alifunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 6-1 waliopata Liverpool dhidi ya Southampton jana na kuiwezesha timu hiyo kutinga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Ligi. Akihojiwa kuhusu kiwango cha Origi, Klopp amesema ni mchezaji mzuri mzuri lakini bdo mdogo hivyo ana vitu vingi vya kujifunza. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa Origi anapaswa kuwa na subira na huo ndio ukweli wenyewe kama anataka afikie mafanikio makubwa.
No comments:
Post a Comment