Thursday, December 3, 2015

ETOILE YATOA USHINDI WAO KWA WALIOKUFA KATIKA SHAMBULIO LA BOMU TUNIS.

KLABU ya Etoile du Sahel Tunisia leo wameutoa ushindi wao wa Kombe la Shirikisho kwa walinzi 12 wa rais waliouawa katika shambulio la bomu jijini Tunis mwezi uliopita. Klabu hiyo yenye maskani yake katika mji wa Sousse, ilishinda taji hilo mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini na kuwafanya kuibuka kidedea kwa jumla ya mabao 2-1 katika michezo miwili waliyokutana. Wakiwa katika mapokezi huko Tunis mbele ya rais wa nchi hiyo Beji Caid Essebsi, kiongozi wa Etoile Ridha Charfeddine amesema wanamkabidhi rais ushindi huo kama heshima kwa walinzi wote waliopoteza maisha kwa tukio la bomu Novemba 24 mwaka huu. Kiongozi huyo aliendelea kudai kuwa sio kwa wachezaji, mashabiki au viongozi, tukio hilo lilikuwa mawazo mwao mpaka dakika za mwisho. Novemba 24 basi lililokuwa limewabeba walinzi maalumu wa rais lililipuliwa katikati ya jiji la Tunis ya kuua 12 kati yao, tukio ambalo Dola Kiislamu-IS walidai kuhusika nalo.

No comments:

Post a Comment