Thursday, December 3, 2015

RATIBA KOMBE LA LIGI.

KLABU ya Liverpool sasa inatarajia kukwaana na Stoke City katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Ligi. Liverpool ilitinga hatua hiyo kwa kishindo kwa kuibamiza Southampton kwa ajumla ya mabao 6-1 katika mchezo wa robo fainali uliochezwa jana. Nusu fainali nyingine ya michuano hiyo itawakutanisha vinara wa Ligi Kuu Manchester City watakaokwaana na Everton. Mechi za nusu fainali ambazo zitakuwa za mikondo miwili zinatarajiwa kuchezwa Januari 4 na Januari 25 huku ule wa fainali ukitarajiwa kuchezwa Februari 28 mwakani.

No comments:

Post a Comment