RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blater ambaye amesimamishwa kwa muda wa siku tisini kutojihusisha na masuala yeyote ya soka, ametaka kifungo hicho kufutwa. Mwanasheria wa kiongozi huyo, Richard Cullen, amesema ushahidi anaonyesha kwamba Blatter alipokuwa ndani ya FIFA hakuwahi kukiuka maadili ya shirikisho hilo. Wakili huyu alikuwa akizungumza baada ya jopo la kamati ya maadili ya FIFA kusema uchunguzi umefungwa. Blatter alifungiwa kwa siku 90 kuanzia Octoba mwaka huu kwa tuhuma za malipo ya dola milioni mbili kwenda kwa rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA Michel Platini, ambae pia amefungiwa kwa sakata hilo.
No comments:
Post a Comment