MKURUGENZI wa ufundi wa Chelsea, Michael Emenalo amesema wachezaji wa timu hiyo hawapaswi kulaumiwa kufuatia kutimuliwa kwa Jose Mourinho. Mabingwa hao watetezi wako alama moja juu ya eneo la kushuka daraja baada ya kupoteza michezo tisa kati ya 16 ya ligi waliyocheza msimu huu. Emenalo amesema kulikuwa na suala la kutoelewana kati ya meneja na wachezaji. Mkurugenzi huyo aliendeela kudai kuwa kama klabu walipaswa walipaswa kufanya jambo ili kujikwamua kutoka katika hali hiyo ndio maana anasisitiza achezaji hawapaswi kulaumiwa kutokana na hilo.
No comments:
Post a Comment