KLABU ya Chelsea imemtimua rasmi kibarua meneja wake Jose Mourinho miezi saba baada ya kuiongoza timu hiyo kunyakuwa ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza. Mourinho mwenye umri wa miaka 52 raia wa Ureno alikuwa akitumikia kipindi cha pili katika klabu hiyo kuanzia Juni mwaka 2013. Chelsea walimaliza ligi msimu uliopita wakiongoza kwa tofauti ya alama tatu na pia kushinda taji la Kombe la Ligi, lakini hali imekuwa tofauti msimu huu wakishindwa kabisa kutetea taji lao kwa kukubali kipigo katika mechi tisa kati ya 16 walizocheza mpaka sasa. Mechi ya mwisho kwa Mourinho ilikuwa kipigo cha mabao 2-1 walichoapa kutoka kwa Leicester City Jumatatu iliyopita. Makocha Pep Guardiola, Guus Hiddink, Brendan Rodgers na Juande Ramos wanatajwa kuchukua nafasi ya Mourinho.
No comments:
Post a Comment