MABINGWA wa Ulaya Barcelona, wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia baada ya kuichapa Guangzhou Evergrande ya China kwa mabao 3-0 katika mchezo wa nusu fainali. Katika mchezo huo Barcelona iliwakosa washambuliaji wake nyota Neymar na Lionel Messi ambao wanasumbuliwa na majeruhi lakini hilo halikuwazuia kupata matokeo waliyohitaji. Mshambuliaji Luis Suarez ndio alikuwa mwiba mchungu kwa Evergrande inayonolewa na kocha wa zamani wa Uingereza Sven-Goran Erikson, kwani ndio aliyefunga mabao yote matatu katika mchezo huo.
Suarez aliifungia bao la kuongoza Barcelona katika dakika ya 39 ya mchezo kabla ya kuongeza lingine dakika ya 50 huku bao la tatu akifunga kwa njia ya penati katika dakika ya 67. Barcelona sasa wanatarajiwa kupambana na River Plate ya Argentina katika mchezo wa fainali unaotarajiwa kufanyika jijini Yokohama, Jumapili hii.
No comments:
Post a Comment