Thursday, December 17, 2015

WINGA WA WEST BROM AMWITA KLOPP MJINGA.

WINGA wa West Bromwich Albion, James McClean amemshambulia meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kwa kumuita mjinga wakati wa mahojiano yake na BBC. Mara kadhaa Klopp alirushiana maneno na meneja wa timu pinzani Tony Pulis katika mchezo baina ya timu hizo uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 Jumapili iliyopita na kupelekea wawili hao kutopeana mikono baada ya kipenga cha mwisho. Meneja huyo raia wa Ujerumani pia alikimbia uwanjani kuchangilia bao la kusawazisha la Liverpool katika dakika za majeruhi na kufuatwa na mmoja kati ya viongozi wa benchi la ufundi la West Brom. Akihojiwa McClean mwenye umri wa miaka 26 amesema anamheshimu sana Klopp kwasababu ya kazi kubwa aliyofanya akiwa Borussia Dortmund lakini anadhani alifanya jambo la kijinga katika mchezo huo. McClean amesema katika mchezo wa Jumapili hakupaswa kufanya alichofanya haijalishi umeshinda, umefungwa au umepata sare huko ni kukoa heshima.

No comments:

Post a Comment