Thursday, December 17, 2015

WENGER AMTETEA HASIMU WAKE MOURINHO.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amekitetea kikosi cha Chelsea chini ya Jose Mourinho akisisitiza kuwa hawataweza kushuka daraja pamoja na magumu wanayopitia hivi sasa. Kibarua cha Mourinho kimekuwa mashakani baada ya kipigo cha mabao 2-1 walichopata kutoka Leicester City Jumatatu na kuiacha Chelsea wakiwa alama moja juu ya eneo la kushuka daraja katika michezo 16 ya ligi waliyocheza mpaka sasa. Chelsea watambana na Sunderland ambao nao wanasuasua katika Uwanja wa Stamford Bridge Jumamosi hii na kipigo kingine kinaweza kuwashuhudia mabingwa hao wakiingia kabisa eneo la kushuka daraja kueleka kipindi kipindi cha Chirstmas. Wenger ambaye kikosi cha kinashika nafasi ya pili msimamo wa ligi amesema haiwezekani kwa Chelsea kushuka daraja. Meneja huyo amesema hadhani kama wako katika hatari ya kushuka daraja hivi sasa kwasababu ya ubora wa kikosi walichonacho.

No comments:

Post a Comment