VYOMBO vya habari nchini Ujerumani, vimeripoti kuwa Pep Guardiola ameiambia Bayern Munich kuwa ataondoka mwishoni mwa msimu huu. Mkataba wa meneja huyo unatarajiwa kumalizika Juni mwakani na Guardiola mwenyewe amesema atatangaza kabla ya Christmas kama ataondoka au kuongeza mkataba. Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na gazeti la kila siku la Bild, Guardiola alishawasilisha uamuzi wake wa kuondoka kwa ofisa mkuu wa Bayern Klarl-Heinz Rummenigge wiki iliyopita. Gazeti hilo liliongeza katika taarifa yake kuwa kila kitu kinaonyesha kuwa Guardiola ataondoka mwishoni mwa msimu. Gazeti lingine la Kicker lenyewe lilidai kuwa kuondoka kwa kocha huyo ni siri ambayo iko wazi.
No comments:
Post a Comment