WINGA wa zamani wa kimataifa wa Ureno, Luis Figo anaamini utulivu huwa haupo pindi unapokuwa kocha wa Real Madrid, kufuatia tetesi juu ya mustakabali wa kibarua cha Rafa Benitez. Shinikizo linazidi kuongezeka kwa Benitez baada ya matokeo kadhaa mabovu katika miezi ya karibuni kikiwemo kipigo cha mabao 4-0 walichopata kutoka kwa mahasimu wao Barcelola katika Clasico. Madrid walichapwa tena bao 1-0 na Villarreal mwishoni mwa wiki iliyopita hivyo kuwafanya kushindwa kupunguza pengo la alama baina yao na vinara wa La Liga Barcelona. Akihojiwa Figo amesema suala la utulivu Madrid halipo kwa meneja yeyote kwasababu kikosi chao kinategemea matokeo mazuri wakati wote hivyo unapokuja katika klabu hiyo lazima ujihadhari na hilo.
No comments:
Post a Comment