Thursday, December 17, 2015

SANCHEZ TAYARI KWA AJILI YA MAN CITY.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa Alex Sanchez yuko tayari kurejea uwanjani wakati timu itakapokwaana na Manchester City katika mchezo wa Ligi Kuu. Nyota huyo wa kimataifa wa Chile, alipata majeruhi ya msuli mwezi uliopita katika sare ya bao 1-1 waliyopata dhidi ya Norwich City lakini ameanza kuonyesha matumaini katika mazoezi wiki hii. Arsenal wanaoshika nafasi ya pili katika msimamo wa ligi wataivaa City walioko chini yao kwa tofauti ya alama moja katika mchezo utakaofanyika katika Uwanja wa Emirates Jumatatu ijayo. Akihojiwa Wenger amesema kuna mchezaji mmoja au wawili ambao wanaweza kurejea na Alex Sanchez ni mojawapo kati ya hao. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa wanahitaji kucheza kwa kiwangi chao cha juu kama watahitaji kuwafunga City hivyo nguvu kazi itahitajika.

No comments:

Post a Comment