POGBA AMMWAGIA SIFA PIRLO.
KIUNGO wa Juventus Paul Pogba amemmwagia sifa mkongwe Andrea Pirlo baada ya kufunga bao kwa mpira wa adhabu katika ushindi wa mabao 4-0 waliopata dhidi ya Torino jana katika mchezo wa Kombe la Italia. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa alifunga bao hilo umbali wa mita 25, na kuihakikishia timu yake ushindi dhidi ya mahasimu wao hao wa jiji. Akihojiwa Pogba alimshukuru Pirlo kwa ushauri aliokuwa akimpatia wakati wakiwa Turin kwani ndio umemsaidia kwa kiasi kikubwa kuwa alivyo sasa. Pogba mwenye umri wa miaka 22 aliendelea kudai kuwa kwasasa wanahamishia nguvu zao katika mchezo wao ujao wa Serie A.
No comments:
Post a Comment