NAHODHA wa zamani wa Cameroon, Samuel Eto’o ameteuliwa kuwa kocha mchezaji wa muda wa klabu ya Antalyaspor ya Uturuki. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye alijiunga na Antalyaspor kwa mkataba wa miaka miatatu Juni mwaka huu, amepewa mechi tatu za kuonyesha uwezo wake katika fani ya ukocha. Eto’o ataiongoza klabu hiyo na kusaidiwa na Mehmet Ugurlu ambaye ni mkurugenzi wa timu hiyo. Klabu hiyo itaamua kama itampa kibarua cha moja kwa moja Eto’o baada ya mapumziko ya majira ya baridi kumalizika.
No comments:
Post a Comment