Wednesday, December 16, 2015

MAZEMBE WAANGUKIA PUA TENA JAPAN.

MABINGWA wa Afrika, TP Mazembe wamechabangwa tena mabao 2-1 na Club America ya Mexico katika mchezo wa kutafuta mshindi tano wa michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia uliofanyika leo huko Japan. Mabao yaliyofungwa na Dario Benedetto na Martin Zuniga katika kipindi cha kwanza yalitosha kuwapata ushindi mabingwa hao wa Concacaf katika mchezo huo. Pamoja na Rainford Kalaba kusawazisha bao moja dakika mbili kabla ya mapumziko lakini Mazembe walishindwa kuizidi maarifa timu hiyo ya Mexico hivyo kuzima ndoto zao za kuondoka na chochote katika michuano hiyo. Jumapili iliyopita Mazembe walitandikwa mabao 3-0 na Sanfrecce Hiroshima katika mchezo wa robo fainali na kuzima ndoto zao za kufika fainali ya michuano hiyo kama walivyofanyika miaka mitano iliyopita.

No comments:

Post a Comment