MUSTAKABALI wa meneja wa Chelsea uko mashakani baada ya viongozi wa klabu kufanya majadiliano kuhusu nafasi hiyo katika kipindi cha saa 24 zilizopita. Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich aliongoza mazungumzo hayo ya jinsi gani mabingwa hao wa Ligi Kuu wataweza kujikwamua kutoka walipo ambapo wamashapoteza mechi tisa kati ya 16 walizocheza mpaka sasa. Chelsea iko alama moja juu ya eneo la kushuka daraja baada ya kutandikwa tena na Leicester City Jumatatu usiku. Katika majadiliano hayo nafasi ya Mourinho ndio imekuwa ajenda kubwa na jinsi watavyoweza kubadili upepo ili timu hiyo iweze kufanya vyema. Kama uongozi wa klabu hiyo ukiamua kumtimua kazi Mourinho, Abramovich atalazimika kumlipa kocha huyo kiasi cha paundi milioni 40.
No comments:
Post a Comment