MENEJA wa Bayern Munich, Pep Guardiola amethibitisha kuwa atatangaza mipango yake ijayo wiki ijayo kufuatia kuzidi kwa tetesi zinazomhusisha na yeye kuwindwa na klabu za Manchester United na Manchester City. Akihojiwa mara baada ya kikosi chake kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Darmastadt katika mchezo wa DFB Pokal, Guardiola alithibitisha kuwa atatoa kauli yake wiki ijayo. Guardiola amesema kwasasa hana majibu ila wiki ijayo maswali yote yatajibiwa ikiwemo suala la muskabali wake. Tayari kumeshakuwa na kauli tofauti kuhusu kocha huyo ambapo kocha wa zamani wa Bayern Ottmar Hitzfeld amesema anategemea Guardiola kukubali kwenda kuinoa City huku Franz Beckernbauer ambaye ni rais wa heshima wa klabu hiyo akidai angefaa zaidi kama angeenda United. Taarifa zingine ambazo zilitawala vyombo vya habari mwishoni mwa wiki iliyopita ni kuwa United walikuwa wameongeza nguvu ya mawasiliano na kocha huyo katika kujaribu kumchukua.
No comments:
Post a Comment