Wednesday, December 16, 2015

CHELSEA SIO YA KUBEZA - YAYA TOURE.

KIUNGO wa Manchester City, Yaya Toure amesema Chelsea ni kama mnyama aliyejeruhiwa na hawapaswi kudharauliwa na wapinzani wao wajao. Chelsea chini ya Jose Mourinho ilipokea kipigo cha cha tisa katika Ligi Kuu msimu huu wakati walipofungw amabao 2-1 na Leicester City Jumatatu usiku. Matokeo hayo yakawafanya mabingwa hao watetezi kuwa katika ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu wakiwa alama moja juu ya eneo la kushuka daraja. Akihojiwa Toure amesema Chelsea kwasasa wanapita katika kipindi kigumu lakini hana shaka kuwa wanaweza kubadili mambo na kupata matokeo mazuri. Kiungo huyo aliendelea kudai pamoja na matatizo waliyonayo hawapaswi kubezwa na wapinzani wao kwani wanaweza kubadilika na kufanya vyema wakati wowote.

No comments:

Post a Comment