RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter aliyesimamishwa, amesema Real Madrid na Atletico Madrid zitakabiliwa na adhabu sawa na Barcelona kama wakikutwa na hatia ya kuvunja sheria ya usajili wa wachezaji chipukizi. Barcelona walifungiwa kusajili wachezaji wapya kwa misimu miwili baada ya kukutwa na hatia ya kuvunja sheria hiyo. Imeripotiwa mapema mwezi Aprili kuwa klabu hizo zinazotoka jiji la Madrid pia azinaweza kukabiliwa na adhabu kufungiwa kusajili kwa mwaka mmoja kutokana na kuhisiwa kuvunja sheria hiyo. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo, Blatter amesema kama timu hizo zikikutwa na hatia hiyo hakuna shaka kuwa watapata adhabu sawa kama aliyopata Barcelona.
No comments:
Post a Comment