Wednesday, December 16, 2015

FC TWENTE YAFUNGIWA MIAKA MITATU.

KLABU ya FC Twente imefungiwa miaka mitatu kushiriki michuano ya Ulaya na Shirikisho la Soka cha Uholanzi. Shirikisho hilo kimedai kupotoshwa kwa makusudi na klabu hiyo kuhusu mpango wa haki za kuuza mchezaji kwa mwekezaji wan je. Taarifa ya klabu hiyo imedai kuwa hawatakata rufani kupinga adhabu hiyo waliyopewa. Shirikisho la Soka la Duniani-FIFA lilifungia suala la mchezaji kuwa na mmiliki wa watu kutokana na tishio la uaminifu kwasababu wawekezaji wangeweza kupandisha ada ya uhamisho ili watengeneze faida. FC Twente pia wametozwa faini ya paundi 34,000 kufuatia klabu hiyo kushindwa kutoa vielelezo vya kutosha kuhusiana na suala hilo.

No comments:

Post a Comment