KAMATI ya waamuzi ya Shirikisho la Ssoka la Ulaya-UEFA imeteua orodha ya waamuzi 18 kwa ajili ya michuano ya Uulaya itakayofanyika nchini Ufaransa mwakani. Waamuzi hao watachezesha michezo 51 ya michuano hiyo itakayoanza kutimua vumbi kuanzia June 10 na kumalizika Julai 10 mwaka 2016. Katika kila mchezo mmoja watatumika waamuzi watano kama ilivyokua katika michuano ya Ulaya mwaka 2012, kutakua na mwamuzi wa kati akisaidiwa na waamuzi wawili wa pembeni na wengine wawili katika kila goli. Orodha ya mwisho ya waamuzi watakaochezesha fainali hizo itatolewa Februari mwakani na kamati hiyo ya waamuzi.
No comments:
Post a Comment