Wednesday, December 16, 2015

FABREGAS AWATAKA WACHEZAJI WENZAKE KUACHA USTAA.

KIUNGO wa Chelsea, Cesc Fabregas amedai kuwa wachezaji wa timu hiyo wanapaswa kuangalia kiasi kikubwa cha mishahara wanayolipwa na kuanza kucheza kama wachezaji wakubwa. Mabingwa hao wa Ligi Kuu wamekuwa wakisuasua msimu huu na kuporomoka mpaka nafasi ya 16 baada ya kukubali kipigo chao cha tisa kutoka kwa Leicester City Jumatatu. Baada ya mchezo huo meneja wa Chelsea alilalamika kazi yake kuhujumiwa na wachezaji wake. Akihojiwa kuhusiana na suala hilo, Fabregas amesema kama ni mchezaji mkubwa na unalipwa mshahara mkubwa unatakiwa kucheza kwa kiwango cha kama hadhi yako ilivyo. Fabregas aliendelea kudai kuwa wanapaswa kucheza kwa kiwango cha juu muda wote ili kuweza kuibeba timu haswa kipindi hiki.

No comments:

Post a Comment