KLABU ya Manchester United inatarajiwa kukwaana na timu ya Midtjylland ya Denmark katika hatua ya timu 32 bora ya michuano ya Europa League baada ya kuondolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp atarejea Ujerumani kwa mara ya kwanza wakati timu yake itakapokwenda kuchuana na Augsburg. Waingereza Tottenham Hotspurs kwa mara nyingine tena wamepangwa kucheza na Fiorentina ya Italia katika hiyo ikiwa ni msimu wa pili mfululizo kwa timu hizzo kukutana. Mechi za mkondo wa kwanza za michuano hiyo zinatarajiwa kuchezwa Februari 18 na 25 huku zile marudiano zikichezwa Machi 10 na 17.

No comments:
Post a Comment