MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema mshambuliaji wake Olivier Giroud anastahili sifa zaidi baada ya kucheza vyema na kuiwezesha timu hiyo kukwea kileleni mwa Ligi Kuu. Nyota huyo wa kimataifa wa Ufaransa alifunga bao la kuongoza kwa penati jana katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Aston Villa, likiwa ni bao lake la 50 katika Ligi Kuu. Giroud pia alifunga hat-trick Jumatano iliyopita katika mchezo wa mwisho wa makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Olympiakos na kutinga hatua ya timu 16 bora. Akihojiwa Wenger amesema Giroud yuko katika kiwango cha juu hivi sasa lakini muda mwingine watu humkosoa. Giroud mwenye umri wa miaka 29 anakuwa mchezaji wa saba wa Arsenal kufunga mabao 50 katika Ligi Kuu.

No comments:
Post a Comment