Tuesday, December 8, 2015

FERGUSON AIPIGIA CHAPUO LEICESTER KUSHINDA TAJI LA LIGI KUU.


MENEJA wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amedai Leicester City ina uwezo wa kushinda taji la Ligi Kuu msimu huu. Leicester ambao wananolewa na Claudio Ranieri wako kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kucheza mechi 15 kwa tofauti ya alama mbili dhidi ya Arsenal wanaoshika nafasi ya pili. Mshambuliaji wake Jamie Vardy ndiye anayeongoza orodha ya wafungaji akiwa na mabao 14, ikiwemo rekodi ya kufunga mabao 11 katika mechi 11 mfululizo na Ferguson anaamini kiwango walichonacho kinaweza kuendelea kwa msimu wote. Akihojiwa Ferguson amesema kwasasa Leicester wako vizuri kwani kikosi chao kina nguvu na kasi na hakuna shaka kwamba ndio timu bora katika ligi.

No comments:

Post a Comment