RAIS wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA, Michel Platini anatarajiwa kujua hatma yake wiki hii kama adhabu ya kusimamishwa siku 90 itaondolewa kwa muda. Platini mwenye umri wa miaka 60, alisimamishwa sambamba na rais wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter Octoba mwaka huu kupisha uchunguzi wa masuala ya rushwa ambao wote walikanusha. Mawakili wake wanatarajiwa kuhudhuriwa usikilizwaji wa rufani ya katika Mahakama ya Michezo ya Kimataifa-CAS leo na uamuzi kutarajiwa kutolewa Ijumaa hii. Platini raia wa Ufaransa anataka kugombea nafasi ya urais wa FIFA lakini amefungiwa kujihusisha na masuala yeyote ya soka. Platini na Blatter wamesimamishwa kufuatia tuhuma za kulipana malipo yasiyo yauaminifu ya paundi milioni 1.3 mwaka 2011 kwa kazi zilizofanyika kati ya mwaka 1998 na 2002.

No comments:
Post a Comment