MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal amesema kikosi kinastahili kuonyesha kuwa wanastahili nafasi ya katika hatua ya timu 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuifunga Wolfsburg katika mechi yao ya mwisho ya makundi. United watafuzu hatua hiyo kama wakishinda mchezo wao wa leo wa kundi B, au PSV Eindhoven wakipoteza mchezo wao dhidi ya CSKA Moscow. Lakini PSV pia anaweza kufuzu kama wakifanikiwa kuyazidi matokeo yeyote watakayopata United katika mchezo wao huko Ujerumani. Akihojiwa kuelekea katika mchezo huo, Van Gaal amesema ni muhimu sana kwa klabu kuendelea katika michuano hiyo na hawawezi kutegemea matokeo kutoka katika mchezo mwingine. United imelenga kutinga hatua ya mtoano ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza toka washindwa kufuzu michuano ya Ulaya chini ya David Moyes msimu wa 2013-2014.

No comments:
Post a Comment