Tuesday, December 8, 2015

MABINGWA WATETEZI ARSENAL KUCHEZA NA SUNDERLAND ROUND YA TATU YA KOMBE LA FA.

MABINGWA watetezi wa Kombe la FA Arsenal, wanatarajiwa kuanza kuteeta taji lao nyumbani kwa mchezo wa mzunguko wa tatu dhidi ya Sunderland. Katika ratiba hiyo kutakuwa mechi tano zitakazohusisha timu za Ligi Kuu ambapo Tottenham Hotspurs wao wamepangwa kucheza na vinara wa ligi Leicester City huku Manchester City mabingwa wa mwaka 2011 wa michuano hiyo wakichuana na Norwich City. Mechi zingine zitawakutanisha Southampton mabingwa wa mwaka 1976 dhidi ya Crystal Palace huku Watford wao wakiwa wenyeji wa Newcastle United. Timu za Ligi Kuu zitakazocheza na timu za madaraja ya chini ni pamoja na Liverpool watakaosafiri kuifuata timu ya daraja la pili ya Two Exeter, wakati Aston Villa wanashikilia mkia katika ligi wakikwaana na Waycombe nayo ya daraja la pili. Manchester United wao watavaana na Sheffield United huku Burnley wakiwa wageni wa Middlesbrough na Swansea City wakiifuata Oxford United.Mechi hizo zinatarajiwa kuchezwa Januari 8 na 11 mwakani.

No comments:

Post a Comment