Friday, December 4, 2015

GARY NEVILLE ATUA VALENCIA.

MENEJA mpya wa Valencia, Gary Neville amesema angekuwa amejipotezea uaminifu kama angekataa nafasi ya kuinoa klabu hiyo ya Hispania. Beki huyo wa zamani wa Manchester United ambaye aligeukia kazi ya uchambuzi aliendelea kudai kuwa amezikataa kazi kadhaa za kufundisha toka alipoamua kutundika daruga zake. Neville mwenye umri wa miaka 40, amesema baada ya kukaa katika luninga kwa miaka kadhaa sasa anadhani wakati muafaka umefika wa kusimama. Neville ambaye pia amekuwa sehemu ya bennchi la ufundi la timu ya taifa ya Uingereza akimsaidia Roy Hodgson, anatarajiwa kuinoa Valencia mpaka mwishoni mwa msimu huu.

No comments:

Post a Comment