Wednesday, December 23, 2015

MENDES AKANUSHA TETESI ZA MOURINHO KWENDA MAN UNITED.

WAKALA wa Jose Mourinho, Jorge Mendes amedai hakuna ofa yeyote rasmi iliyotolewa na Manchester United kwa ajili ya kumchukua kocha huyo. Mendez amesema hajui litakalotokea siku zijazo lakini kwasasa hakuna makubaliano yeyote wala ofa yeyote rasmi iliyokuja. Mourinho alitimuliwa na Chelsea wiki iliyopita, miezi saba baada ya kuingoza timu hiyo kunyakuwa taji la Ligi Kuu. Kocha huyo Mreno ambaye amewahi kunyakuwa matatu ya Ligi Kuu akiwa na Chelsea alishatoa taarifa akisisitiza kuwa hana mpango wa kupumzika.

No comments:

Post a Comment