Wednesday, December 23, 2015

SKRTEL NJE WIKI SITA.

BEKI wa Liverpool, Martin Skrtel amethibitisha kuwa anatarajia kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha wiki sita kutokana na mejeruhi. Nyota huyo wa kimataifa wa Slovakia mwenye umri wa miaka 31, alitolewa akiwa anachechemea katika dakika ya 44 ya mchezo wa Ligi Kuu ambao walitandikwa mabao 3-0 na Watford Jumapili iliyopita. Skrtel aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwa alichanika msuli wa nyuma ya paja katika mchezo huo. Beki huyo aliendelea kudai kuwa anafahamu itakuwa ni safari ndefu kuelekea kupona lakini atafanya kila awezalo kuhakikisha anarejea haraka iwezekanavyo. Skrtel amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Liverpool msimu huu akiwa amecheza mechi 26 za mashindano yote.

No comments:

Post a Comment