Wednesday, December 23, 2015

WENGER AMKINGIA KIFUA VAN GAAL.

MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger ameelezea tetesi zinazoendelea zikimhusisha Jose Mourinho kuchukua nafasi ya Louis van Gaal Manchester United, kuwa ni ukosefu wa heshima. Mourinho alitimuliwa Chelsea Alhamisi iliyopita baada ya mabingwa hao kushindwa kufanya vyema toka kuanza kwa msimu. Hata hivyo, kocha huyo Mreno toka wakati huo amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Old Trafford kufuatia shinikizo kubwa alilonalo Van Gaal ambaye ameshindwa kupata ushindi katika mechi zake sita zilizopita za mashindano yote. Akiulizwa kuhusu kuondoka kwa Mourinho, Wenger amesema anadhani vingi vimezungumzwa lakini ukweli ni kwamba huwa hapendi mtu apoteze kibarua chake. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa ana heshima kubwa kwa Van Gaal na kinachoendelea dhidi yake kwasasa sio heshima.

No comments:

Post a Comment