Wednesday, December 23, 2015

GUARDIOLA ANA UWEZO WA KUFUNDISHA POPOTE DUNIANI - RONALDINHO.

NYOTA wa zamani wa Barcelona, Ronaldinho amedai kuwa Pep Guardiola ana uwezo wa kufundisha soka popote duniani. Klabu ya Bayern Munich ilitangaza mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa Guardiola hataongeza mkataba wake na mabingwa hao wa Bundesliga huku Manchester City, Manchester United na Chelsea zikitajwa kuwania saini yake msimu ujao. Baada ya kunyakuwa mataji matatu ya La Liga, mawili ya Kombe la Mfalme na mawili ya Ligi ya mabingwa Ulaya akiwa na Barcelona, Guardiola amekuwa akibeba taji la Bundesliga toka atue Bayern ingawa bao hajapata taji la Ulaya akiwa Ujerumani. Popote atakapokwenda, Ronaldinho ambaye aliondoka Barcelona muda mfupi baada ya Guardiola kuteuliwa mwaka 2008, anategemea kocha huyo kuendelea kupata mafanikio. Ronaldinho amesema Guardiola ni kocha mkubwa ambaye ana uweze wa kufundisha timu yeyote duniani.

No comments:

Post a Comment