Wednesday, December 23, 2015

KOMPANY KUREJEA BOXING DAY.

MENEJA wa Manchester City Manuel Pellegrini amesema nahodha wake Vincent Kompany anaweza kurejea uwanjani katika mchezo dhidi ya Sunderland utakaofanyika Boxing Day. Kompany amekosa mechi tano za Ligi Kuu za City kutokana na majeruhi ya nyonga ambapo timu hiyo ilipoteza michezo mitatu kati ya hiyo na kushinda miwili na kuwafanya kuwa nyuma ya vinara Leicester City kwa alama sita. City imeshapoteza mechi tano jumla msimu huu lakini hawajafungwa wakati Kompany akiwa uwanjani. Pellegrini ana matumaini beki huyo wa kimataifa wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 29 atarejea katika kikosi cha kwanza katika mchezo huo wa Ligi Kuu. Kocha huyo amesema Kompany amekuwa akifanya mazoezi na kikosi cha kwanza kwa siku mbili zilizopita hivyo ana matumaini Jumamosi hii anaweza kuwa fiti kwa kucheza.

No comments:

Post a Comment