Wednesday, December 23, 2015

BRADLEY MCHEZAJI BORA WA MWAKA MAREKANI.

NAHODHA wa timu ya taifa ya Marekani, Michael Bradley ametajwa kuwa mwanasoka wa mwaka wa nchi hiyo jana. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 28 ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka, kufuatia mafanikio ambayo amepata katika klabu yake na mechi za kimataifa. Akiwa nahodha wa Toronto FC amefainikiwa kuisaidia klabu hiyo kucheza hatua ya mtoano ya Ligi Kuu ya Marekani-MLS kwa mara ya kwanza katika historia yao. Mkongwe huyo ambaye amecheza katika fainali mbili za Kombe la Dunia alitimiza mechi yake ya 100 akiwa na kikosi cha Marekani na kuwa mchezaji wanne mdogo kufikia hatua hiyo.

No comments:

Post a Comment