Wednesday, December 23, 2015

VERON ADAI MESSI ANAPENDA KUCHEZA INTER.

MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Argentina, Juan Sebastian Veron amesema Lionel Messi alishawahi kumdokeza kuwa anataka kuichezea Inter Milan. Nyota huyo wa Barcelona maisha yake yote ya soka amekuwa akiitumikia klabu hiyo lakini amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwindwa na vilabu kadhaa katika miaka ya karibuni. Na Veron ambaye amewahi kucheza katika klabu za Sampdoria, Parma, Lazio na Inter katika kipindi chake cha miaka 20 aliyocheza soka, amesema Messi alishawahi kumwambia kuhusu nia yake ya kwenda kucheza Inter. Veron aliendelea kudai kuwa ni miaka mingi imepita lakini kuna wakati nyota huyo alishawahi kumuambia angependa kucheza Inter.

No comments:

Post a Comment