Friday, December 4, 2015

MESSI AFIKISHA FOLLOWERS MILIONI 30 INSTAGRAM.

MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amefanikiwa kutimiza idadi ya mashabiki milioni 30 wanaomfuata katika mtandao wa kijamii wa Instagram jana na ametumiwa pongezi na mchezaji nyota wa mpira wa kikapu wa timu ya Golden State Warriors, Stephen Curry. Kufuatia mafanikio hayo, Messi alituma picha katika mtandao huo akionyesha fulana ya Barcelona yenye namba 30 mgongoni ambayo aliivaa katika mchezo wa la Liga kwa mara ya kwanza akiwa na timu hiyo. Picha hiyo ya Messi ilikwenda sambamba na ujumbe wa kuwashukuru mashabiki wake hao kwa kumuunga mkono kwa kipindi chote hicho. Lakini pamoja na hayo, Messi pia alipongezwa na Curry ambaye alimualika kwenda kushuhudia moja ya mechi za Golden State Warroirs siku za mbeleni.

No comments:

Post a Comment