MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amesema hana tatizo kama wakosoaji watamlaumu yeye kwa majeruhi ya msuli wa paja aliyopata Alexis Sanchez. Nyota huyo wa kimataifa wa Chile alitolewa katika kipindi cha pili katika mchezo waliotoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Norwich City Jumapili iliyopita baada ya kupata majeruhi. Hatua hiyo inakuja ikiwa imepita wiki moja toka Wenger akiri kuwa Sanchez alikuwa akihitaji mapumziko. Muda halisi ambao Sanchez atakaa nje ya uwanja haujafahamika lakini wadau wanakadiria inaweza kuwa mwezi mmoja. Wenger amesema kama mtu yeyote anataka kumlaumu kwa kuumia kwa nyota huyo ni sawa kwake kwani hana tatizo.
No comments:
Post a Comment