KIUNGO wa Liverpool, James Milner amesema meneja wao Jurgen Klopp amewaletea imani mpya katika kikosi chao toka achukue mikoba ya kuwafundisha Octoba mwaka huu. Klopp amepoteza mchezo mmoja pekee ambao walifungwa mabao 2-1 na Crystal Palace toka achukue mikoba hiyo kutoka kwa Brendan Rodgers. Kwasasa Liverpool imetinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Ligi kwa ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya Southampton. Milner ambaye amechukua mikoba ya unahodha kutokana na kukosekana kwa Jordan Henderson, amekiri kuwa Liverpool ilikuwa inakosa kujiamini kabla ya ujio wa Klopp. Kiungo huyo wa kimataifa wa Uingereza amesema kwasasa anaona taratibu hali ikibadilika na hali ya kujiamini kuingia katika kikosi chao.

No comments:
Post a Comment