WINGA wa Real Madrid, gareth Bale amesisitiza uhusiano wake na Cristiano Ronaldo na meneja wao Rafa Benitez ni imara. Nyota huyo wa kimataifa wa Wales alifunga bao wakati Madrid wapofanikiwa kuvuka kikwazo cha wiki mbili ngumu kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Getafe jana katika Uwanja wa Santiago Bernabeu. Akihojiwa kuhusu uhusiano wake na Ronaldo pamoja na Benitez, Bale amesema wachezaji wote katika kikosi hicho wanaelewana vyema. Bale aliendelea kudai kuwa ni vyema kwani anajisikia huru anapokuwa na wachezaji wa kikosi chao na wanaelewana vyema kabisa na Ronaldo na Benitez. Nyota huyo amesema pamoja na kuenguliwa katika michuano ya Kombe la Mfalme lakini mashabiki bado wameendelea kuwaunga mkono na wamefuhishwa na ushindi waliopata.

No comments:
Post a Comment