MENEJA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amesema kupata kwao ushindi katika mechi moja kati ya nne za Ligi Kuu zilizopita kunatokana na kubakiwa na wachezaji kati ya 13 au 14 waliokuwa fiti. Yaya Toure, Sergio Aguero, Vincent Kompany, Pablo Zabaleta na Samir Nasri wote waliokosa mchezo wa jana ambao walitandikwa mabao 2-0 na Stoke City, wakati Fernando alipata majeruhi ya msuli wa paja. City walitangaza kikosi cha Ligi Kuu cha wachezaji 21 Septemba mwaka huu, wakipungukiwa wachezaji wanne kutimia idadi kamili ya wachezaji 25. Pellegrini amesema wamekuwa wakicheza na wachezaji walewale katika mechi zao tatu zilizopita ndio maana anadhani walishindwa kucheza katika kiwango kilichohitajika. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa tatizo kubwa linawakabili hivi sasa ni kushiriki katika mashindano mengi halafu wachezaji haohao ndio wanaotumika hivyo lazima uchovu uwaingie kwakuwa hawapati muda wa kutosha kupumzika.

No comments:
Post a Comment