Sunday, December 6, 2015

RAMSEY AFURAHIA NAFASI MPYA ALIYOPEWA NA WENGER.

KIUNGO wa Arsenal, Aarone Ramsey amedai kufurahishwa na nafasi ya kiungo wa kati aliyopewa wakati timu hiyo ikikwea mpaka nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu kufuatia ushindi wa mabao 3-1 waliopata dhidi ya Sunderland jana. Nyota huyo wa kimataifa wa Wales alitengeneza bao pili lililofungwa na Olivier Giroud kabla ya kufunga bao lingine mwenyewe katika dakika za majeruhi na kuihakikishia Arsenal ushindi huo muhimu ambao umewafanya kutofautiana na vinara Leicester City kwa alama mbili. Kuumia kwa Santi Cazorla na Francis Coquelin kumemfanya Ramsey kupata nafasi ya kucheza nafasi ya kiungo wa kati na kukiri kuwa anajisikia vyema kurejea katika nafasi anayoipenda. Ramsey amesema anajisikia huru zaidi akicheza nafasi hiyo kwani inaendana na mchezo wake vyema.

No comments:

Post a Comment