TIMU ya taifa ya Nigeria imefanikiwa kuichapa Algeria kwa mabao 2-1 na kutwaa taji la michuano ya Mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya umri wa miaka 23 katika mchezo wa fainali uliofanyika jijini Dakar, Senegal jana. Katika mchezo huo Nigeria walichukua uongozi wa mapema kwa bao la penati lilifungwa na nahodha Peter Etebo dakika ya 14 kabla Algeria nao hawajasawazisha dakika 16 baadae kufuatia bao la kujifunga la Oduduwa Segun Tope. Nigeria walifanikiwa kuchukua uongozi tena mwishoni mwa kipindi kipindi cha kwanza kupitia kwa yuleyule nahodha wake Etebo mabao ambayo yalidumu mpaka mpira unamalizika. Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu, Afrika Kusini ilifanikiwa kuwazima wenyeji Senegal kwa kuwatandika kwa changamoto ya mikwaju ya penati 3-1 na kuikwaa nafasi ya kushiriki michuano ya Olimpiki itakayofanyika jijini Rio de Janeiro, Brazil mwakani. Afrika Kusini wataungana na mabingwa Nigeria pamoja na washindi wa pili wa michuano hiyo Algeria kwenda kushiriki mashindano hayo.

No comments:
Post a Comment