Sunday, December 13, 2015

VAN GAAL AWATAKA WACHEZAJI KUUNGANA.

MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal amekitaka kikosi chake kuungana pamoja wakati akijipanga kutafuta ushindi katika mechi tatu mfululizo ili kuwabakisha katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu. Kipigo cha mabao 2-1 walichopata kutoka kwa Bournemouth jana kimeifanya United kuwa wameshinda mechi mbili pekee kati ya saba za ligi walizocheza. Kwasasa wanashiklilia nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi, akiwa nyuma ya vinara Manchester City kwa alama tatu. Akihojiwa Van Gaal amesema kupoteza michezo miwili mfululizo ni jambo la kusikitisha, sasa wanatakiwa kuendelea kupambana ili kubaki katika nafasi. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa wanapaswa kushinda mechi tatu mfululizo ili kuweza kubaki katika nafasi za juu baada ya Christmas.

No comments:

Post a Comment