Sunday, December 27, 2015

ROBINHO ATAMANI KUREJEA BRAZIL.

MSHAMBULIAJI mkongwe wa kimataifa wa Brazil, Robinho amesema anaweza kurejea kucheza soka nchini kwao pindi mkataba wake na mabingwa wa soka wa Asia Guangzhou Evergrande utakapomalizika. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31 amefunga mabao matatu katika mechi tisa za ligi alizoichezea Guangzhou toka aliposaini mkataba wa miaka miezi sita na timu hiyo inayonolewa na Luis Felipe Scolari. Hata hivyo, Robinho amesema anataka kurejea Brazil ambako alicheza katika timu ya Santos katika msimu wa 2014-2015 kwa mkopo akitoke AC Milan ya Italia. Mkongwe huyo aliendelea kudai kuwa hilo ni jambo analofikiria lakini bado hajaamua chochote mpaka sasa kwani anafurahia mapumziko yake ya sikukuu.

No comments:

Post a Comment