Sunday, December 27, 2015

KLOPP AKIRI HAIKUWA KAZI RAHISI KUIFUNGA LEICESTER CITY.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amekipongeza kikosi chake kwa kushinda mchezo wao dhidi ya vinara wa Ligi Kuu Leicester City jana katika Uwanja wa Anfield. Kabla ya mchezo huo wa jana ambao walishinda bao 1-0, Liverpool walikuwa wameambulia alama moja katika mechi tatu zilizopita za ligi. Lakini Liverpool walionekana kubalika kabisa katika mchezo huo wa jana ambao bao pekee liliwekwa kimiani na Christian Benteke aliyeingia akitokea benchi katika kipindi cha pili. Akihojiwa Klopp amesema kuwafunga vinara wa ligi ni kazi ngumu kwani timu nyingi ziejaribu lakini zimeshindwa ndio maana anafurahia ushindi kwakuwa walistahili. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa walikuwa na subira jambo ambalo limewasaidia kwa kiasi kikubwa katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment