Monday, December 28, 2015

TUNACHEZA KWA AJILI YA VAN GAAL - CARRICK.

KIUNGO wa manchester United, Michael Carrick amesema madai ya kuwa wachezaji wa timu hiyo hawajitumi ili kulinda kibarua cha meneja wao Louis van Gaal, ni kuwakosea heshima. Kipigo walichopata United Jumamosi iliyopita kinakuwa cha nne mfululizo na kuendelea rekodi yao kutoshinda katika mechi saba. Van Gaal ambaye amesema anaweza kujiuzulu alikuwa katika uwanja wa mazoezi wa United jana. Carrick amesema ni suala la ukosefu wa heshima watu kudai kuwa hawajitumi kwa ajili ya meneja wao ni jambo linalowaumiza kwani wao sio watu wa aina hiyo. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa anafahamu kama ilivyo kwao matokeo yanawaumiza lakini sio kweli kuwa hawajitumi kwani wanafanya kila wawezali wakishirikiana vyema na meneja kubadili hali ilivyo.

No comments:

Post a Comment