Monday, December 28, 2015

POCHETTINO AWAZODOA WANAOMUWINDA KANE.

MENEJA wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino amesisitiza Harry Kane hatauzwa kwa bei yeyote ile. Kane alifunga bao lake la 10 na 11 msimu huu katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata dhidi ya Norwich City Jumamosi iliyopita na kuwa mchezaji wa kwanza wa Spurs kufunga mabao 27 au zaidi kwa mwaka. Kiwango cha Kane katika kipindi cha miezi 12 iliyopita pia kimemfanya kuitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza, huku vilabu kadhaa vikubwa vikimmezea mate zikiwemo Manchester United na Chelsea. Hata hivyo, Pochettino amesisitiza kuwa hakuna klabu itakayoweza kumnunua nyota huyo kwasasa kwani ni muhimu katika kikosi chao. Meneja huyo amesema hakuna kiwango cha bei alichowekewa hivyo haitawezekana kununuliwa kwasasa.

No comments:

Post a Comment