Monday, December 28, 2015

RONALDO ATASTAAFU AKIWA NA UMRI WA MIAKA 40 - MENDES.

WAKALA wa mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo amedai kuwa nyota huyo bado ataendelea kuitumikia timu hiyo mpaka atakapofikisha miaka 40. Ronaldo mwenye umri wa miaka 30 na mshindi wa tuzo tatu za Ballon d’Or amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Paris Saint-Germain au klabu yake ya zamani ya Manchester United kabla hajatundika daruga zake. Nyota huyo wa kimataifa wa Ureno ana mkataba na Madrid unaomalizika Juni mwaka 2018, lakini Mendes amesisitiza mteja wake bado anaweza kuendelea kubakia Santiago Bernabeu kwa muongo mwingine mmoja. 
Jorge Mendes akipokea tuzo ya wakala bora wa mwaka katika sherehe za Globe Soccer zilizofanyika huko Dubai jana.
Mendes amesema Ronaldo ndio mchezaji bora wa wakati wote na ana uhakika kuwa anaweza kucheza kwa miaka mingine zaidi ya saba akiwa Madrid. Wakala huyo aliendelea kudai kuwa ana furaha kuitumikia klabu hiyo na atastaafu akiwa na umri wa miaka 40.

No comments:

Post a Comment